Star Boy anawasubiri Singida BS Ijumaa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 May 2026
Star Boy anawasubiri Singida BS Ijumaa

Ijumaa mashabiki wa Yanga watakuwa na matumaini makubwa kwa kiungo mshambuliaji Allain Okello wakati timu hiyo itakaposhuka dimbani kuivaa Singida Black Stars katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa mjini Singida uliisha kwa Yanga kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0, ulikuwa mchezo maalum kwa nyota huyo kutoka Uganda. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Okello kuifungia Yanga kwenye ligi tangu alipojiunga na mabingwa hao watetezi.

Bao hilo lilikuwa mwanzo wa safari mpya ya mafanikio kwake ndani ya kikosi cha Yanga.

Tangu siku hiyo, Okello amegeuka kuwa silaha muhimu kwa Yanga. Kiungo huyo amekuwa akionyesha kiwango cha juu kwa kufunga mabao saba na kutoa pasi saba za magoli, takwimu zinazothibitisha mchango wake mkubwa katika harakati za timu hiyo kutetea ubingwa.

Katika hatua hii ya mwisho ya msimu, presha imeongezeka zaidi kwa Yanga. Hakuna nafasi ya kufanya makosa tena ikiwa wanataka kubaki kileleni na kutwaa ubingwa wa tano mfululizo.

Kila mchezo uliobaki umebeba uzito wa fainali, na mchezo dhidi ya Singida BS ni mmoja wa mechi zinazoweza kuamua hatma ya ubingwa.

Kipigo cha mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji FC kimewapa matumaini wapinzani wao wakubwa Simba ambao sasa wanaamini mbio za ubingwa bado ziko wazi.

Hata hivyo, ukweli unabaki kuwa Yanga bado wanashikilia hatma yao wenyewe. Wakifanikiwa kushinda mechi zao zote zilizobaki, hawatahitaji kutegemea matokeo ya timu nyingine ili kutwaa tena taji la ligi.

Ijumaa inaweza kuwa siku nyingine kwa “Star Boy” kuendeleza makali yake akishirikiana na kina Pacome Zouzoua, Muthathir, Prince Dube na mastaa wengine kuhakikisha mipango ya Yanga kutetea ubingwa inabaki salama.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’