Kikosi cha Yanga leo kitahitimisha maandalizi yake kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida BS ambao utapigwa kesho Ijumaa, May 22 uwanja wa KMC Complex.
Kocha Abdihamid Moalin na vijana wake walirejea mazoezini siku ya Jumanne kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo pamoja na mchezo utakaofuata dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa siku ya Jumatatu.
Zikiwa zimesalia mechi 7 kukamilisha msimu, kila mchezo kwa Yanga sasa ni fainali kwani makosa yoyote yanaweza kuwanufaisha watani zao Simba ambao leo watacheza dhidi ya Coastal Union na pengine kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa saa 24 kabla ya mchezon dhidi ya Yanga hapo kesho.
Meneja wa habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri kuelekea mchezo huo akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi dimba la KMC Complex hapo kesho kuwaongezea hamasa wachezaji wao.
Mchezo dhidi ya Singida BS unatarajiwa kupigwa saa 10 jioni..