Moalin afunguka maandalizi ya kuikabili Singida BS

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 May 2026
Moalin afunguka maandalizi ya kuikabili Singida BS

Kocha Mkuu wa Yanga Abdihamid Moalin amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida BS yanakwenda vizuri ambapo leo watakamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho Ijumaa, May 22 katika uwanja wa KMC Complex.

Licha ya kuwaheshimu Singida BS kutokana na ubora wa kikosi chao, Moalin amesema mchezo huo ni muhimu sana kwa Yanga na mkakati wao ni kuhakikisha wanapata ushindi.

"Maandalizi yanaendelea vizuri na leo tutafanya mazoezi yetu ya mwisho, tunawaheshimu Singida BS kwa sababu tunajua ni timu ngumu yenye ushindani mkubwa, lakini sisi kama Yanga tunajua umuhimu wa mchezo huu na malengo yetu ni kupata alama tatu," alisema Moalin.

Katika mechi za karibuni Yanga imetengeneza nafasi nyingi lakini ufanisi umekuwa mdogo mbele ya lango. Moalin amesema ni jambo jema kwao kutengeneza nafasi hizo kwani anaamini uwezekano wa kufunga mabao mengi pia unakuwa mkubwa.

"Ni kweli, mchezo uliopita tulitengeneza nafasi nyingi sana za mabao na hilo ni jambo zuri kwa timu. Ni kweli hatukufanikiwa kutumia nafasi zote tulizopata, lakini hiyo ni sehemu ya kawaida ya mchezo wa soka. Tulipoteza kwa makosa lakini tulifanikiwa kwa namna timu ilionesha uhitaji wa alama tatu kwa kutengeneza nafasi nyingi."

“Wachezaji ni binadamu na kuna nyakati mambo hayaendi kama wanavyotaka, kitu muhimu ni kuendelea kuwaamini na kuwapa sapoti muda wote,hata sisi binafsi kwenye maisha yetu ya kawaida huwa kuna nyakati tunaanguka."

"Kwenye soka jambo muhimu ni kutengeneza nafasi nyingi za mabao, ukiendelea kutengeneza nafasi nyingi uwezekano wa kufunga mabao mengi unakuwa mkubwa zaidi. Tukisema tuanze hapa kuhesabu makosa ya mchezaji mmoja mmoja tunapoteza muda. Watakosa leo na kesho watakosa tena ni kawaida ya mchezo wa Soka, muhimu ni kuendelea kutengeneza nafasi nyingi. Huwezi kukwepa makosa kwenye soka,” alisema

Yanga inahitaji kushinda mchezo dhidi ya Singida BS ili kulinda malengo yake ya kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’