Mlinzi wa Yanga Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema wanauchukulia kila mchezo kwa uzito mkubwa ili kuhakikisha wanatetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.
Zimbwe Jr ambaye alikuwa nje kwa wiki kadhaa akiuguza majeraha amesema matokeo ya mchezo uliopita yamewakumbusha ugumu ulioko mbele yao hasa baada ya gap la pointi kati yao na Simba kubaki mbili.
Amesema wamepata muda wa kufanya tathmini na kubaini walipokosena na sas watachukua tahadhari kuhakikisha hawafanyi makosa zaidi.
“Tunachukua tahadhari zote kwa kila mchezo ambao unakuja mbele yetu, tulikuwa na uwiano wa tofauti ya alama tano sasa zimebaki alama mbili."
"Huu ni ujumbe wa tahadhari kwetu, bila shaka tumepata nafasi ya kujitafakari na kujua wapi tulipokosea”
“Kuelekea kwenye mbio za ubingwa kesho alama tatu kwetu ni muhimu mno, hatuna cha kujitetea au kujifichia wapinzani wetu kwa sababu wametukaribia sana. Muhimu ni kuwa na umakini mkubwa ili tuweze kutimiza malengo haya,” alisema Zimbwe Jr ambaye msimu uliopita alikuwa nahodha wa Simba