Uongozi wa klabu ya Yanga umewakumbusha wanachama kuwa Mkutano Mkuu wa klabu hiyo unaofanyika kesho Jumapili Juni 10, 2018 katika ukumbi wa Bwalo la Polisi Masaki jijini Dar es salaam, utaanza saa nne kamili asubuhi.

Wanachama wamesisitiziwa kulipia ada zao za mwaka, wale ambao hawatakuwa wamelipia hawataruhusiwa kushiriki.
Mapema leo idadi kubwa ya wanachama wa Yanga walioneka Benki ya Posta jijini Dar es salaam wakilipia ada zao tayari kwa Mkutano huo muhimu kwa mustakabali wa klabu ya Yanga.

ADVERTISE HERE