Mlinzi wa kushoto wa Yanga Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema changamoto ya majeraha imemfanya akosekane kwenye baadhi ya mechi lakini sasa anaendelea vyema na atarejea kikosini siku za karibuni.
Kukosekana kwa beki huyo aliyejiunga na Yanga Julai 2025 akitokea klabu ya Simba, kuliibua propaganda mitandaoni zikisambazwa taarifa hachezi kwa sababu ana madai Yanga.
Licha ya Meneja wake kutoa ufafanuzi hivi karibuni, Zimbwe Jr amesisitiza kuwa hana tatizo lolote na uongozi wa Yanga na kilichomuweka nje ni changamoto ya mejaraha tu.
"Hayo mambo mengine ni propaganda tu, mimi sidai wala sina tatizo na kiongozi yeyote, niko freshi kabisha."
"Tatizo ambalo nilikuwa nalo ni majeraha ndio maana watu wengi ambao walizoea kuniona mara kwa mara nikicheza, hawakuniona na ndio sintofahamu zilipoanzia lakini sidai wala sina tatizo na kiongozi yeyote, namshukuru Mungu kwa hilo"
"Kwa sasa ninaendelea vizuri na Wanayanga watarajie kuniona uwanjani siku si nyingi," alisema Zimbwe Jr.
Zimbwe Jr ameungana na wachezaji wengine wakiweka msimamo kuwa jukumu lao ni kuhakikisha wanatetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo hivyo watahakikisha wanashinda mechi 6 zilizobaki