GSM ameweka 'mzigo' wa maana kutetea ubingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 May 2026
GSM ameweka 'mzigo' wa maana kutetea ubingwa

Jana Yanga ilirejea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuichapa Namungo Fc mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.

Yalikuwa matokeo muhimu kwa Yanga kurejea kwenye nafasi hiyo kabla ya mapumziko ya kalenda ya FIFA ambayo yatachukua takribani wiki mbili.

Wakati wa kusaini makubaliano ya ujenzi wa Yanga na GSM, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said aliweka wazi kuwa malengo makuu ya Yanga ni kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo. Hersi aliwahakikishia Wananchi kuwa timu yao inakwenda kutetea ubingwa.

Tangu Hersi atoe kauli hiyo Yanga imeandikisha ushindi kwenye kila mchezo wakizifunga Singida BS (3-0) na Namungo Fc (3-1).

Inaelezwa Mfadhili/Mdhamini wa Yanga GSM ameweka bonasi kwa kila ushindi katika mechi 7 za mwisho. Ambapo kama Yanga itashinda mech zote zilizosalia na kutetea ubingwa, watakusanya kiasi kikubwa cha fedha.

Mmoja wa wachezaji wandamizi ndani ya kikosi amefichua mpango huo wa bonasi ambapo kama wataukamilisha vyema, wataweza kuvuna zaidi ya Tsh Milioni 700.

“Tumeambiwa kwamba tunachotakiwa kukipigania ni ubingwa na sio rekodi ya kutokufungwa, tajiri anataka kuona tunashinda hizi mechi zilizosalia,” amesema mmoja wa mastaa wa timu hiyo.

“Kwenye kila mchezo kuanzia ile ya Singida, tumeambiwa tukishinda tu thamani yake ni Sh100 milioni, kwahiyo kwa mechi hizi zilizosalia kama tukishinda zote, basi tutachukua jumla ya Sh700 milioni,” alidokeza

Yanga imebakisha mechi 5 kutetea ubingwa wake ambapo baada ya mapumziko ya FIFA, Juni 13 itakuwa mkoani Kigoma kuikabili Mashujaa Fc.

Baada ya mchezo huo wataelekea mkoani Arusha kuikabili Fountain Gate Juni 17 na kisha kurejea jijini Dar es salaam kumaliza msimu kwa mechi dhidi ya Azam Fc, TRA United na JKT Tanzania

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’