Kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello amepewa medali ya ubingwa wa ligi kuu ya Uganda msimu huu na klabu yake ya zamani Vipers Fc.
kabla ya kujiunga na Yanga mwezi Januari 2026 kwenye usajili wa dirisha dogo, Okello alikuwa sehemu ya kikosi cha Vipers akiifungia timu hiyo mabao matatu.
Vipers Fc ambao wametwaa taji la ligi kuu ya Uganda, wamethibitisha kuwa Okello atapata medali.
Star Boy anaweza kuondoka na medali mbili za ubingwa msimu huu kama atafanikiwa kuiongoza Yanga kutetea taji la ligi kuu.
Yanga jana ilirejea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo Fc Okello akiweka kambani mabao mawili.
Okello ameifungia Yanga mabao 11 na kutoa pasi 7 za mabao akihusika katika mabao 18.
ADVERTISE HERE