Mshambuliaji wa Yanga Laurindo Aurelio 'Depu' amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Angola kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Botswana na Central Africa.
Depu alikuwa mshambuliaji tegemeo wa kikosi cha Angola wakati timu hiyo ikinolewa na aliyekuwa kocha wa Yanga Pedro Goncalves.
Licha ya kutokuwa na nyakati nzuri kwa sasa kwenye kikosi cha Yanga, kocha wa Angola, Aliou Cisse ameamjumuisha kwenye kikosi chake.
Nyota wengine wa Yanga ambao watakuwa na majukumu kwenye timu za Taifa katika kipindi hiki cha mapumziko ya FIFA ni Djigui Diarra, Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Mudathir Yahya, Allan Okello na Prince Dube.
Depu alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akipachika mabao 11 katika mechi 10 za kwanza katika mashindano yote.
Hata hivyo alipata majeraha ambayo yalimfanya akosekane kwa wiki kadhaa.