Kikosi cha Yanga Princess kimeendelea kupotea njia kwenye ligi kuu ya Wanawake jana wakilazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Fountain Gate Princess.
Huo ulikuwa mchezo wa tatu mfululizo Yanga Princess inakosa ushindi kwenye ligi kuu ya Wanawake ambayo inaelekea ukingoni.
Ni kama timu ilipoteza muelekeo baada ya kupigo cha mabao 2-1 dhidi ya Simba Queens, kwani baada ya matokeo hayo hawakuweza tena kupata ushindi.
Kabla ya mchezo dhidi ya Fountain Gate, wametoka kupoteza mchezo dhidi ya Mashujaa Queens ukiwa ni mchezo wa tatu wanapoteza msimu huu.
Mpaka kukamilika duru ya kwanza, kulikuwa na matarajio makubwa kwa Yanga Princess kwenye mbio za ubingwa kwani walikuwa nafasi ya pili kwa tofauti ya alama moja tu dhidi ya Simba Queens.
Lakini sasa wameachwa alama 10 na watani zao hao ambao ni wazi msimu huu watatwaa ubingwa.
Kuna jitihada kubwa uongozi wa Yanga ulifanya mwanzoni mwa msimu wakiimarisha kikosi lakini inaonekana bado upande wa timu ya Wanawake, Yanga haijajipata.