Mafanikio ya timu ni kipaumbele - Moallin

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 May 2026
Mafanikio ya timu ni kipaumbele - Moallin

Katika mechi nne mfululizo kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello amefunga mabao mawili kila mechi mashabiki wakitamani kuona mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uganda anapewa muda zaidi wa kucheza ili afunge hat-trik ya kwanza msimu huu.

Hata hivyo imekuwa tofauti, mara nyingi benchi la ufundi la Yanga humtumia Okello kwa tahadhari, kwani ni nadra kwake kumaliza dakika 90. Kocha Abdihamid Moalin amefichua mpango wa kumlinda star huyo ili kumuepusha na majeraha

Moallin amesema wanatambua kiu ya mashabiki lakini kwa sasa kuna haja ya kuangalia mafanikio ya jumla ya timu na sio rekodi binafsi katika mechi zilizosalia.

“Nikweli najua mashabiki wanatamani hilo, lakini kwa sasa timu yetu lazima tuwe makini, tumemkosa Pacome (Zouzoua) baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Singida, wote tunafahamu umuhimu wa kuwa na Pacome kwenye timu yetu,” amesema Moallin.

“Hatuwezi kufanya kosa lingine kwa kuruhusu kuumia kwa Okello wakati ambao ameshatekeleza vizuri lengo kuu la timu kushinda, tulichotakiwa ni kuulinda ushindi wetu, tuna sababu ya kuangalia mbele zaidi.

“Hatuzuii wachezaji kuweka rekodi binafsi, ikitokea wamefanya hivyo wote tutafurahia lakini kitu muhimu hapa kwetu kwasasa ni kuangalia mafanikio ya timu kwa ujumla ambayo ni kushinda ubingwa msimu huu,” alisema Moallin

Kuhusu Pacome, Moallin amewahakikisha mashabiki wa Yanga kuwa atarejea kwa wakati na pengine watamuona uwanjani kwenye mchezo utakaofuata (dhidi ya Mashujaa Fc) baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA

“Pacome atarejea kwa wakati, alishaanza matibabu ya eneo ambalo ameumia, tunatarajia atakuwa tayari kabla ya kwenda kucheza mchezo unaofuata ugenini, pia nadhani kuna wengine nao watakuwa wamekaa sawa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’