Baada ya mapumziko ya wiki nzima, kikosi cha Yanga leo kinarejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya meechi za mwisho ya kuhitimisha msimu.
Mwezi huu msimu wa ligi kuu na kombe la CRDB unafika tamati ambapo Yanga inakwenda kupambania kutetea mataji yote mawili.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji wote ambao hawana majukumu ya timu za Taifa wataanza kujifua leo dimba la KMC Complex.
Wananchi watakuwa na zaidi ya siku 10 za kujiandaa kabla ya kuelekea mkoani Kigoma kuikabili Mashujaa Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Lake Tanganyika, Juni 13.
Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea mkoani Arusha kuikabili Fountain Gate, Juni 17.
ADVERTISE HERE