Ni mechi tano za kusaka ubingwa na heshima

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jun 2026
Ni mechi tano za kusaka ubingwa na heshima

Msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara umekuwa wa ushindani mkali. Yanga ikichuana vikali na watani zao Simba kuwania taji la ligi kuu.

Wananchi wako kileleni wakiwa na alama 60 huku Simba ikiwa nafasi ya pili ikiwa na alama 55 huku kila timu ikisalia na mechi tano.

Kwa Yanga, ubingwa unaweza kuwa na uzito mkubwa zaidi kuliko misimu ya nyuma, kutokana na mazingira hayo ya ushindani.

Msimu uliopita bado unabaki kuwa moja ya misimu bora zaidi katika historia ya klabu hiyo. Yanga ilitwaa ubingwa ikiwa na rekodi ya alama 82 pamoja na kufunga mabao 83, takwimu ambazo zimeweka kiwango cha ubora katika ligi.

Licha ya malengo ya kutetea taji, Yanga haitoweza kufikia au kuvunja takwimu za msimu uliopita. Katika mechi tano zilizobaki, hata kama watafanikiwa kushinda zote, watafikisha alama 75, ambayo ni pungufu ya kile walichokipata msimu uliopita.

Vivyo hivyo, kwenye upande wa mabao, timu hiyo kwa sasa ina mabao 58, ikiwa nyuma kwa zaidi ya mabao 25 ukilinganisha na msimu uliopita.

Licha ya kushuka kwa takwimu, malengo makuu ya msimu huu kwa Wananchi ni wazi: kutetea taji la ligi kwa mara ya tano mfululizo. Hili ni jambo ambalo bado lina uzito mkubwa na linaweza kuingia katika historia ya mafanikio ya klabu.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Yanga kufikia mafanikio ya kutwaa mataji mfululizo kwa misimu mingi, lakini kufanya hivyo katika mazingira ya sasa ya ushindani mkali kunalifanya jambo hilo kuwa na thamani zaidi.

Uwepo wa ushindani mkali kutoka kwa wapinzani wao wa jadi Simba, umeufanya msimu huu kuwa mgumu zaidi. Hali hiyo inamaanisha kuwa endapo Yanga watafanikiwa kutetea taji, ubingwa huo utakuwa wa heshima kubwa zaidi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’