Habari njema kwa Wananchi kuelekea mechi za mwishoni mwa msimu, ni kurejea kikosini kwa mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' ambaye alikuwa nje kwa wiki kadhaa akiuguza majeraha.
Zimbwe Jr sasa yuko fit akishiriki kikamilifu mazoezi na wachezaji wengine chini ya makocha Abdihamid Moalin na Patrick Mabedi.
Leo wachezaji wa Yanga walifanya 'session' mbili ambapo asubuhi kulikuwa na program maalum ya mazoezi ya Gym.




ADVERTISE HERE