Mzize anarejea akiwa Imara zaidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jun 2026
Mzize anarejea akiwa Imara zaidi

Mashabiki wa Yanga wanaweza kutabasamu baada ya mshambuliaji wao Clement Mzize, kuonyesha maendeleo makubwa katika safari yake ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa sehemu kubwa ya msimu huu.

Mzize tayari ameanza programu za mazoezi ya Gym ikiwa ni sehemu ya hatua za mwisho za kurejea kwake uwanjani. Hata hivyo, uongozi wa Yanga hauna mpango wa kuharakisha kurejea kwake kwenye ushindani wa mechi rasmi, ukitaka kumpa muda wa kutosha kujiimarisha kimwili na kuhakikisha anarejea akiwa katika kiwango bora kabisa bila hatari ya kupata majeraha mengine.

Safari ya majeraha ya mshambuliaji huyo ilianza wakati wa michuano ya CHAN iliyofanyika mwezi Agosti 2025 katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania. Akiwa na kikosi cha Taifa Stars, Mzize alipata tatizo la goti ambalo lilimfanya kukosa mechi kadhaa za mwanzo wa msimu wa Yanga.

Baada ya matibabu na programu za uangalizi, alifanikiwa kurejea uwanjani, lakini bahati mbaya majeraha hayo yalitoneshwa tena na kumlazimu kukaa nje kwa kipindi kingine. Licha ya changamoto hiyo, jitihada za kumpa matibabu ziliendelea na mshambuliaji huyo akarejea kwa mara nyingine, akicheza kwa dakika chache katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FAR Rabat nchini Morocco.

Hata hivyo, baada ya mchezo huo hali yake haikuwa nzuri tena na majeraha yakajirudia. Kutokana na hali hiyo, Yanga iliamua kuchukua hatua ya ziada kwa kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu maalum ambapo alifanyiwa upasuaji mwingine wa goti ili kutatua tatizo hilo kwa kiwango cha kudumu.

Kwa sasa maendeleo ya Mzize ni vizuri na amebakiza hatua chache kabla ya kurejea kwenye mazoezi ya kawaida ya mpira. Hata hivyo, viongozi wa Yanga wanaamini hakuna sababu ya kuhatarisha afya yake kwa kumrudisha haraka, hasa ikizingatiwa historia ya majeraha aliyopitia katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kwa mujibu wa ratiba ya urejeaji wake, mashabiki wa Yanga wanatarajiwa kumuona tena Mzize uwanjani wakati wa maandalizi ya msimu mpya (pre-season), ambapo atapata nafasi ya kurejesha makali yake taratibu kabla ya kuanza kutumika kikamilifu katika mashindano ya msimu ujao.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
26m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
45m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
50m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’