Usajili Yanga utazingatia maeneo haya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jun 2026
Usajili Yanga utazingatia maeneo haya

Klabu ya Yanga SC ipo katika mchakato wa kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, ambapo taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa uongozi umeweka mkazo mkubwa katika kusajili wachezaji wapya katika maeneo matatu muhimu: ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

Kwa mujibu wa taarifa, Yanga inatafuta beki mmoja wa kati mzawa, viungo wawili wakabaji, pamoja na viungo washambuliaji wawili wa nafasi ya namba 10 na mawinga. Aidha, klabu hiyo pia inalenga kusajili washambuliaji wawili, mmoja mzawa na mwingine wa kigeni.

Katika eneo la kiungo mkabaji, Yanga imeweka mkazo maalum kutokana na pengo lililoachwa na kiungo Khalid Aucho, ambaye aliondoka baada ya mkataba wake kumalizika. Uongozi wa Yanga umeona kuwa klabu haijapata mchezaji aliyefikia kiwango na mchango wa Aucho, hivyo kuamua kuwekeza zaidi katika eneo hilo.

Katika safu ya ulinzi, Yanga inalenga kuongeza beki mmoja wa kati mzawa ili kuongeza ushindani na uimara. Mabeki waliopo kwa sasa ni pamoja na Ibrahim Abdullah ‘Bacca’, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Frank Assink.

Taarifa imebainisha kuwa endapo beki mzawa atapatikana, huenda klabu ikaachana na Assinksi ili kutumia nafasi yake kusajili mchezaji wa kigeni kuboresha maeneo mengine.

Kwa upande wa kiungo mshambuliaji, Yanga inalenga mchezaji namba 10 atakayesaidiana na Allan Okello, ambaye ameanza kuonyesha kiwango bora katika kikosi hicho. Uongozi unaamini ushindani katika nafasi hiyo utaongeza ubora wa timu.

Katika eneo la mawinga, Yanga imekiri kukumbwa na changamoto kwa misimu kadhaa mfululizo, ambapo baadhi ya wachezaji waliowasajili hawajatoa mchango uliotarajiwa. Hivyo klabu inalenga kusajili winga mmoja mwenye kasi na uwezo wa kuwatengenezea nafasi washambuliaji.

Aidha, katika safu ya ushambuliaji, Yanga inalenga kuongeza washambuliaji wawili ili kuimarisha eneo hilo. Klabu inarudi sokoni kupata straika wa kiwango cha juu, licha ya changamoto za gharama za wachezaji wa aina hiyo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’