Mchezo wa ligi kuu ya vijana U17 kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa TFF Kigamboni, umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.
Vijana wa Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 15 kupitia kwa Issa Ramadhani kabla ya Simba kusawazisha dakika za lala salama kupitia Faudh Mohamed.
Ulikuwa ni mchezo ulijaa ufundi mwingi vijana wa Yanga wakionekana kuiva sawasawa kwenye kutandaza soka la kitabuni.
Yanga inaendea kuwekeza kwenye soka la vijana, ni suala la muda vijana, kina Clement Mzize wengi wataandaliwa.
Matokeo ya mchezo huo yanaifanya Yanga U17 isalie nafasi ya tatu ikifikisha alama 13 huku Simba U17 wakiongoza ligi na alama 17. Hata Ynga ina mchezo mmoja wa kiporo.

ADVERTISE HERE