Kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mabingwa hao wa Tanzania Bara kwa mwezi May 2026.
Tuzo hiyo inayodhaminiwa na NIC, ilitarajiwa kuchukuliwa na Okello kutokana na mambo makubwa aliyofanya mwezi May.
Katika mwezi huo Okello aliweka rekodi ya kufunga mabao 9 na kutoa pasi moja ya bao huku akifunga mabao nane katika mechi nne mfululizo.
Okello pia anapigiwa chapuo kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi katika mwezi huo, takwimu zake zikimpa kila sababu ya kushinda tuzo hiyo.

ADVERTISE HERE