Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Azam Fc uliopangwa kupigwa Juni 24, utachezwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
Yanga ndio wenyeji wa mchezo huo muhimu kwa Yanga ambao ushindi utawaweka Wananchi katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa.
Kamwe amesema Yanga tayari imewataarifu Bodi ya ligi juu ya uamuzi wa kuchagua uwanja huo.
Kamwe amesema baada ya mchezo wa nusu fainali kombe la CRDB dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Juni 21 uwanja wa CCM Kirumba, kikosi kitaelekea visiwani Zanzibar tayari kwa mtanange huo wa pili dhidi ya Azam Fc katika kipindi cha siku tatu.
ADVERTISE HERE