Yanga ndiyo timu bora mpaka sasa, takwimu zinajieleza zenyewe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jun 2026
Yanga ndiyo timu bora mpaka sasa, takwimu zinajieleza zenyewe

Kwa muda mrefu katika msimu huu wa 2025/26, kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu kiwango cha Yanga. Wapo wanaosema timu imeporomoka, wengine wakidai ubora wa kikosi umepungua, huku baadhi wakisisitiza kuwa wananchi hawachezi soka la kuvutia kama walivyokuwa wamezoeleka katika misimu iliyopita.

Lakini jambo moja ambalo halipingiki ni kwamba mpira wa miguu hauamuliwi kwa hisia, bali kwa matokeo na takwimu. Na ukiziangalia takwimu za msimu huu kwa jicho la haki, Yanga ndiyo timu bora zaidi mpaka sasa.

Klabu ambayo imekuwa ikikosolewa mara kwa mara ndiyo inayoendelea kuongoza katika maeneo mengi muhimu ya ushindani. Wakati wengine wakizungumzia hisia zao kuhusu kiwango cha timu, Yanga imekuwa ikijibu uwanjani kwa ushindi, pointi na mafanikio ya wachezaji wake mmoja mmoja.

Moja ya viashiria vikubwa vinavyoonyesha ubora wa timu ni uwezo wake wa kuzalisha wachezaji wanaofanya vizuri mara kwa mara. Ndiyo maana tuzo za Mchezaji Bora wa Mwezi zina uzito mkubwa katika kutathmini uimara wa kikosi.

Katika miezi tisa ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26, Yanga imefanikiwa kutoa washindi wa tuzo hiyo mara tano. Hii si bahati mbaya, bali ni uthibitisho wa ubora wa kikosi chao na mwendelezo wa kiwango kizuri cha wachezaji wake.

Safari hiyo ilianza mwezi Septemba 2025 ambapo kipa mahiri Djigui Diarra alitwaa tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora kilichowasaidia wananchi kupata matokeo mazuri. Mwezi Desemba 2025, Duke Abuya naye aliibuka mshindi wa tuzo hiyo baada ya mchango mkubwa alioutoa ndani ya kikosi.

Mwezi Februari 2026, mshambuliaji Laurindo Depu aliendeleza ubabe wa wananchi kwa kutwaa tuzo hiyo, kabla ya Allan Okello kuandika historia yake mwenyewe kwa kushinda tuzo za Aprili na Mei 2026 mfululizo.

Ukiziangalia tuzo zote za msimu huu mpaka sasa, picha inakuwa wazi kabisa:

Septemba 2025 – Djigui Diarra (Yanga)

Oktoba 2025 – Issa Abushiri (Fountain Gate)

Novemba 2025 – Fabrice Ngoy (Namungo)

Desemba 2025 – Duke Abuya (Yanga)

Januari 2026 – William Edgar (Dodoma Jiji)

Februari 2026 – Laurindo Depu (Yanga)

Machi 2026 – Ibrahim Imoro (Singida BS)

Aprili 2026 – Allan Okello (Yanga)

Mei 2026 – Allan Okello (Yanga)

Hii ina maana kwamba kati ya miezi tisa iliyochezwa, Yanga imetawala miezi mitano. Hakuna timu nyingine iliyofikia kiwango hicho msimu huu.

Takwimu hizi zinaonyesha jambo moja muhimu sana; Yanga si timu inayotegemea mchezaji mmoja. Kila kipindi kuna mchezaji tofauti anayesimama na kuibeba timu. Leo ni Djigui Diarra, kesho ni Duke Abuya, baadaye ni Laurindo Depu, halafu Allan Okello. Huu ndiyo utambulisho wa timu kubwa yenye kikosi kipana na chenye ushindani wa ndani.

Kwa kawaida, timu ambayo imepoteza ubora wake haiwezi kuwa na wachezaji wengi wanaoshinda tuzo za mtu binafsi kwa msimu mmoja. Timu ambayo imeporomoka haiwezi kuendelea kutengeneza mastaa wanaotambulika kila mwezi. Lakini Yanga imefanya hivyo tena na tena.

Ukiachana na tuzo hizo, Yanga ndio vinara wa ligi kuu wakiwa na alama 63, alama mbili mbele ya watani zao Simba wanaoshika nafasi ya pili.

Ndio timu iliyofunga mabao mengi zaidi (60) na kuruhusu mabao machache 9 wakiwa sawa na Azam Fc. Yanga ina GD ya mabao 51 wakati Simba iliyo nafasi ya pili ina GD ya mabao 36.

Ikitokea Yanga na Simba zikalingana pointi mwishoni mwa msimu ni wazi Yanga itaibuka na ubingwa iwe kitazingatiwa kigezo cha GD au H2H. 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
9h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
13h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
14h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
14h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’