Tuko tayari kuendeleza ushindi dhidi ya Azam Fc - Moalin

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jun 2026
Tuko tayari kuendeleza ushindi dhidi ya Azam Fc - Moalin

Kocha wa Yanga Abdihamid Moalin amesema ni heshima kwa timu hiyo kucheza mechi ya nusu fainali ya kombe la CRDB kwa msimu wa sita mfululizo, malengo yao ni kushinda mchezo na kutinga fainali.

Azingumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo dhidi ya Azam Fc, Moalin amewapongeza wachezaji wa Yanga kwa kuendelea kuwa washindani na kiu kubwa ya kushinda mataji.

Amesema hawapaswi kuchoka kushinda kwani mbele yao wana jukumu kubwa la kuendeleza umahiri wao na kuandika historia ya kipekee.

"Tumewasili salama na maandalizi ya mchezo wa kesho yanaendelea vizuri. Wachezaji wako katika hali nzuri kiakili na kimwili na tunafahamu kile kinachohitajika kufanyika."

“Ni heshima kubwa kucheza nusu fainali ya mashindano kama haya. Tumestahili kufika hapa lakini lengo letu ni kufika fainali. Ili kufanya hivyo, tunapaswa kuwa bora katika wakati huu na kushinda kesho"

“Jambo kubwa kuhusu kikosi hiki ni kwamba wachezaji wetu wamepitia nyakati kama hizi hapo awali. Wamecheza mechi kubwa, wamekabiliana na presha kubwa na wamefanikiwa. Tunahitaji tu kukumbuka uzoefu huo."

"Tunapaswa kubaki wanyenyekevu, wenye njaa ya mafanikio na tusichoke kushinda. Mara zote huwa nawaambia wachezaji wangu msichoke kushinda, kwa sababu kushinda ni jambo la kipekee ambalo timu nyingi zinatamani kulifikia. Tumeshinda mataji hapo awali, lakini huu ni mwaka mwingine na fursa nyingine ya kuandika historia mpya na tunataka kufanya hivyo tena.”

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa taaluma yao na kujitoa kwao. Kila wanapoingia uwanjani wanapigania nembo ya klabu hii na ninaamini watafanya hivyo tena kesho. Mashabiki wetu ni sehemu muhimu ya mafanikio yetu. Tunahitaji sauti zao, nguvu zao na sapoti yao. Kesho zaidi kuliko wakati mwingine wowote, tunawahitaji wajitokeze kwa wingi na kusimama pamoja nasi,” alisema Moalin

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
28m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
46m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
51m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’