Yanga leo imepoteza mchezo wa nusu fainali kombe la CRDB dhidi ya Azam Fc ikikubali kipigo cha mabao 3-2.
Baada ya ushindi wa mechi 28 mfululizo katika michuano hiyo, hatimaye leo Yanga imeonja kipigo cha kwanza baada ya takribani miaka minne na miezi 10 kupita.
Sio matokeo yanayoweza kuwafurahisha mashabiki lakini ni matokeo ya mpira wa miguu, kuna ushindi, sare au kupoteza.
Leo Yanga ilitoka nyuma mara mbili kuweka mzani sawa lakini haikuwezekana mara ya tatu. Ni sahihi pia kusema ilikuwa siku mbaya ofisinimsafu ya ulinzi hawakuwa kwenye ubora wao.
Bado msimu haujamalizika, kazi kubwa imebaki kutetea taji la ligi kuu. Mbele yuko Azam FC, ushindi dhidi yao utaiweka Yanga kwenye nafasi nzuri ya kurejesha taji Jangwani kwa msimu wa tano mfululizo.
Unaweza kusema mchezo dhidi ya Azam Fc ni kama fainali nyingine, wakati huu hakuna nafasi ya kufanya makosa.