Yanga yaondoka Mwanza, kituo kinachofuata Zanzibar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jun 2026
Yanga yaondoka Mwanza, kituo kinachofuata Zanzibar

Baada ya kumalizana na Azam Fc jana katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la CRDB ambao Wananchi walikubali kipigo cha mabao 3-2, kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Mwanza kurejea Dar es salaam kabla ya kuunganisha kuelekea Zanzibar tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc.

Siku ya Jumatano, dimba la New Amaan Complex litashuhudia dakika nyingine 90 za mchezo kati ya miamba hao ambao jana dakika 120 ziliamua ushindi kwa Azam Fc.

Wakati huu Yanga inahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi.

Ni mechi tatu tu zilizobaki kuhitimisha msimu huu, baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc Yanga itarejea jijini Dar es salaam kuhitimisha mechi nyingine mbili dhidi ya TRA United (KMC Compex) na JKT Tanzania (Isamuhyo).

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wanapaswa kusahau matokeo ya mchezo uliopita haraka ili kuunganisha nguvu kuelekea mchezo wa Jumatano ambao una umuhimu mkubwa.

"Wananchi bado mechi 3 tumalize Ligi Kuu. Mpaka sasa tupo kileleni kwa Tofauti ya pointi 2, kosa moja tu, litatuweka kwenye hatari ya kupoteza Kombe letu la Ligi Kuu"

"Tuinue vichwa vyetu juu,  tuanze maandalizi ya nguvu mapema kwenye mchezo wa Jumatano pale Zanzibar. Mpinzani aliyetuliza leo (jana) hapa Mwanza, tuna dakika 90 dhidi yake tena pale New Amaan Complex."

"Wachezaji wetu wanatuhitaji sana sana Jumatano. Kama uko Bara, uko Pemba, Uko Unguja.. weka ratiba yako vizuri Jumatano YANGA wote Tunakutana New Amaan Complex! Tunatakiwa kuungana na kuwa na morali moja, kushinda Jumatano. ITS A DO or DIE MATCH," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’