Kiungo mshambuliaji wa Al Ittihad Stephane Aziz Ki tayari yuko nchini ambapo jana alikuwa mkoani Dodoma kushiriki mwaliko kutoka kwa Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde.
Taarifa iliyotolewa Mh. Mavunde jana imebainisha kuwa Aziz Ki akiungana nao kutembelea Kijiji cha Matumaini kilichopo Kisasa Jijini,Dodoma kuwaona watoto yatima.
"Leo mimi na Aziz Ki tumepata nafasi ya kutembelea Kijiji cha Matumaini kilichopo Kisasa Jijini,Dodoma kuwaona watoto yatima na kutumia nafasi hiyo pia kutoa sadaka yetu kwa ajili ya watoto hao."
"Pia tumetembelea Hospital ya Rufaa ya Mkoa kuangalia jengo la mapumziko la wananchi wanaokuja kuwaangalia wagonjwa wao ambalo Aziz Ki na Djigui Diarra walichangia kulijenga kwa kuchangia mifuko ya saruji," aliandika Mh. Mavunde kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
Klabu ya Yanga imepiga hatua kubwa kwenye mchakato wa kunmrejesha kiungo mshambuliaji huyo ambaye kabla ya kutimkia Wydad na baadae kujiunga na Al Ittihad mapema mwaka huu, aliitumikia Yanga kwa misimu mitatu.
Wakati huu Yanga ikijipanga kwa maboresho makubwa, Aziz Ki ni miongoni mwa wachezaji ambao mashabiki wengi wanatamani arejeshwe.




