Tutaimaliza kazi hapa Zanzibar - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jun 2026
Tutaimaliza kazi hapa Zanzibar - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe mara baada ya kuwasili Zanzibar, amesema kikosi hicho kimewasili Zanzibar kikiwa na lengo moja tu la kuhakikisha kinatwaa taji la NBC Premier League na kufuta maumivu ya kupoteza mbele ya Azam FC kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank.

Akizungumza baada ya kuwasili visiwani humo jana, Kamwe alisema Azam FC wamebaki na simulizi pekee baada ya ushindi wao wa hivi karibuni, huku akisisitiza kuwa Yanga ipo tayari kumalizia kazi kwenye mchezo ujao.

"Tumeshakula ng'ombe mzima, mkia tu ni kidogo sana na tumejipanga kumalizia sehemu iliyobaki," alisema Kamwe akimaanisha kuwa hatua iliyobaki kuelekea ubingwa si kubwa ukilinganisha na kazi ambayo tayari wameifanya msimu mzima.

Yanga inakabiliwa na mtihani mgumu mbele ya Azam FC ambao tayari wameonyesha uwezo wao wa kuwazuia Wananchi baada ya ushindi wa mabao 3-2 katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Swali kubwa kwa sasa ni je, Azam FC wataweza kuibuka washindi kwa mara ya pili mfululizo dhidi ya Yanga katika Uwanja wa New Amaan Complex, au Wananchi watatumia mchezo huo kuthibitisha ubora wao na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwa msimu wa tano mfululizo?

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 10 jioni muda ambao mechi zote za mzunguuko wa 28 zitapigwa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’