Kabla ya mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya TRA United uliopigwa uwanja wa KMC Complex jana, kuna watu waliweka 'mitego' wakiamini Yanga inaweza kudondosha alama katika mchezo huo.
Kulikuwa na vitisho, tambo lakini Wananchi walitinga KMC Complex wakiwa watulivu na baada ya dakika 90 wakaondoka na ushindi wa mabao 3-0 kiungo mshambuliaji Allan Okello akifunga hat-trik.
Kilichovutia zaidi ni kazi nzuri iliyofanywa na mlinzi wa kushoto Chadrack Boka ambaye alimdhibiti ipasavyo winga tegemeo wa TRA United Ramadhan Chobwedo.
Unaweza kusema Chobwedo ambaye inaelezwa tayari amesajiliwa na Simba, alipewa kazi ngumu ambayo aliishindwa kabla ya kuianza.
Hakuna safari ambayo Chobwedo aliweza kuifanya upande wa Boka zaidi ni yeye aliyekuwa na jukumu la kumkaba Boka ambaye kila mara alipepea kwenye kibendera cha kona akimwaga majaro.
Boka ameendelea kuwashawishi mabosi wa Yanga kuwa bado anastahili kuwatumikia vinara hao wa ligi wanaosaka taji la tano mfululizo.
Mkataba wake unaelekea ukingoni na bado 'anasikilizia' simu ya Injinia Hersi kwa ajili ya mkataba mpya