Ukizungumzia wachambuzi mahiri wa soka nchini hutakosa kutaja jina la Edo Kumwembe, mwandishi mkongwe wa habari za michezo.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Intagram, Kumwembe amewashangaa baadhi ya Waandishi wenzie ambao wanawapa nafasi wapinga mabadiko katika vyombo vyao vya habari.
"Wakati wa Mabadiliko katika klabu zetu umefika kwa ajili ya mambo haya kuwa endelevu. Simba na Yanga zinahitaji mabadiliko ya kudumu ya uendeshwaji," ameandika Kumwembe.
"Nashangaa sana kwa Vyombo vya habari kutoa nafasi kwa wazee wachache sana ambao wanawapinga matajiri kama MO na Yusuf Manji.
"Kitu cha muhimu cha kuzua mjadala ni namna ya kuwakabidhi hizi timu na si eti kulalamika 'tunauza' timu
"Wakati huo huo tunaendelea kushabikia akina Manchester United, Arsenal, Barcelona kwa nguvu wakati zinaendeshwa kwa mifumo hii hii tunayotaka kuwapa akina Manji watuendeshe.
"Sitatoa nafasi kwa mtu anayepinga Mabadiliko, nitatoa nafasi kwa mtu anayetaka kuelimisha jinsi ya kufanya Mabadiliko!"
Kumekuwa na baadhi ya waandishi wa habari 'sote tunawafahamu' ambao wamekuwa wakitumia vyombo vyao vya habari kuwapa nafasi wapinga mabadiliko katika klabu ya Yanga hasa Mzee Akilimali.
Wengine wamekuwa wakimtumia Mzee Akilimali kama chanzo cha habari za klabu ya Yanga licha ya kufahamu yalipo Makao Mkuu ya Yanga kupata taarifa sahihi.

ADVERTISE HERE