Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube mkataba wake na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara umemalizika huku ikielezwa amepata ofa kutoka klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya uongozi wa Yanga, imebainisha kuwa Dube amewaomba viongozi wa Yanga aruhusiwe akatafute changamoto nje ya nchi baada ya kuitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa katika misimu miwili.
Hata hivyo imeelezwa kuwa uongozi wa Yanga bado una nia ya kuendelea nae na wako tayari kumshawishi ili asalie Jangwani.
Msimu huu Dube amefunga mabao 10 lakini akiwa mchezaji tegemeo kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga.
Tofauti na washambuliaji wengi, Dube anaweza kutumika katika maeneo tofauti kwenye safu ya ushambuliaji.
Katika mechi za mwishoni mwa msimu, Dube ametumika zaidi kama mshambuliaji anayetokea pembeni akihusika kwenye mabao yaliyofungwa katika mechi dhidi ya Azam Fc na JKT Tanzania iwe kwa kufunga au kutoa pasi za mabao.
Klabu za nyumbani kwao Zimbabwe Hardrock Fc na Scottland Fc nazo zinatajwa kumuwania mshambuliaji huyo ambaye pia amekuwa mwenendo mzuri kwnye majukumu ya timu ya Tafa ya Zimbabwe.