Mkutano Mkuu Yanga ni August 02

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jul 2026
Mkutano Mkuu Yanga ni August 02

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ametangaza kuwa Mkutano Mkuu wa kawaida wa Wanachama wa Yanga utafanyika Jumapili, August 02 2026.

Miongoni mwa ajenda zitakazojiri kwenye mkutano huo ni uchaguzi mkuu wa klabu kama ilivyoanishwa kwenye taarifa iliyotolewa kwa UMMA.

TAARIFA KWA UMMA

Rais wa Young Africans Sports Club anapenda kuwatangazia wajumbe wote wa Mkutano Mkuu ya kuwa, kutakua na Mkutano Mkuu wa kawaida utakaofanyika siku ya Jumapili tarehe 02/08/2026 kuanzia saa nne (04:00) kamili asubuhi. Hii ni kwa mujibu wa ibara ya 20 ya Katiba ya Young Africans Sports Club ya mwaka 2021.

Mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Super Dome uliopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Ajenda za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:

  1. Kufungua Mkutano
  2. Uhakiki wa wajumbe wanaohudhuria mkutano.

  3. Kuthibitishe Ajenda.

  4. Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita.

  5. Yatokanayo na kumbukumbu za mkutano uliopita.

  6. Hotuba ya Rais.

  7. Kupokea na kujadili taarifa za kazi kutoka Kamati ya Utendaji.

  8. Kuthibitisha hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka uliotangulia, pamoja na kusomewa mapato na matumizi ya Klabu.

  9. Kuthibitisha bajeti kwa mwaka unaofata.

  10. Kupitia mapendekezo ya uwekezaji.

  11. Kupitia Mapendekezo ya marekebisho ya Katiba.

  12. Uchaguzi Mkuu wa Klabu

  13. Mengineyo

  14. Kufunga Mkutano

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’