Wakati Wananchi jana wakisherehekea taji la tano mfululizo ligi kuu ya Tanzania Bara, rekodi nyingine ya kibabe wameiweka kwenye michuano ya kombe la Shirikisho (CRDB) tangu michuano hiyo iliporejea mwaka 2015.
Baada ya kusimama mwaka 2003, michuano hiyo ilirejea mwaka 2015 na walikuwa ni Yanga walioikaribisha kwa kuibuka washindi wakiichapa Azam Fc mabao 3-1 kwenye mchezo wa fainali.
Katika miaka 10 ya michuano hiyo, Yanga imeibuka washindi mara tano huku wakiweka rekodi ya kushinda taji hilo mara nne mfululizo.
Watani zao Simba ambao leo wameweka rekodi ya kufanya paredi la ushindi wa taji hilo, wamechukua mara nne.
Azam Fc imechukua mara moja kama ilivyo kwa Mtibwa Sugar waliochukua taji hilo mara moja pia.
Baada ya kulipoteza msimu huu, Wananchi wameapa msimu ujao wanalirejesha Jangwani kwa mara nyingine