Kocha Mkuu wa Yanga Abdihamid Moalin ametwaa tuzo ya kocha bora wa ligi kuu kwa mwezi Juni 2026.
Mwezi Juni Moalin aliongoza Yanga katika mechi tano ambazo Wananchi walikusanya alama 15 kwa kushinda zote.
Kikosi chake kilifunga mabao 13 bila ya kuruhusu bao lolote ndani ya ligi kuu ya NBC.
Matokeo yaliisaidia Yanga kutwaa taji la ligi kuu ya NBC kwa msimu wa tano mfululizo.
Tuzo ya mchezaji bora imechukuliwa na Ndumumwe Mossi wa Singida BS ambaye mwezi Juni alifunga mabao 8 zikiwemo hat-trik 2.

ADVERTISE HERE