Mshambuliaji wa Gor Mahia Meddy Kagere amesema yuko tayari kutua Yanga kwa dau la Mil 180 pamoja na mshahara wa Mil 11 kwa mwezi.
Mshambuliaji huyo aliye mwishoni mwa mkataba wake katika klabu ya Gor Mahia, amesema hatakuwa na pingamizi kwa timu nyingine yoyote itakayokuwa tayari kutoa dau hilo.
Hata hivyo Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kiasi hicho cha pesa anachotaka Kagere ni kikubwa sana na huenda Yanga ikaachana na mpango wa kumsajili.
Baada ya kutangaza kuunda Kamati Maalum ya kusimamia usajili, Yanga imepania kusajili wachezaji wenye uwezo wa juu ili kuirejeshea timu hiyo makali yake.
Yanga tayari imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Kimataifa wa Benin Mrcelin Koukpo aliyetua nchini hivi karibuni.
Kabla ya kuondoka kurejea kwao DR Congo kwa mapumziko, kocha Mkuu wa Yanga Zahera Mwinyi alisema wanakusudia kusajili wachezaji wengine wanne wa Kimataifa katika nafasi za beki, kiungo, winga na mshambuliaji.

ADVERTISE HERE