Klabu ya Yanga SC inatajwa kuwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Al-Merrikh SC, Aboubakar Bachir Bangoura, imefahamka.
Nyota huyo wa Guinea mwenye umri wa miaka 20 alikuwa na msimu bora wa 2025/26, akitangazwa kuwa Mchezaji Bora Al Merrikh akiibuka kinara wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi.
Winga huyo ana kasi, uwezo wa kupiga chenga na mchango wake mkubwa katika safu ya ushambuliaji, akipachikwa jina la utani "Vinicius Jr wa Guinea".
Kiwango chake bora kimezifanya klabu kadhaa kuanza kumfuatilia, huku Yanga SC ikitajwa kuwa miongoni mwa zinazotaka huduma yake katika dirisha hili la usajili.
Yanga imeweka nguvu kubwa kuimarisha eneo la washambuliaji wa pembeni ikihusishwa pia na winga wa Kaizer Chiefs Makabi Lilepo na winga wa Al Hilal Jean Claude Girumugisha.