Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto ni mchezaji huru baada ya ya mkataba wake wa mabingwa hao wa soka Tanzania Bara kufikia tamati.
Meneja wa mchezaji huyo Carlos 'Mastamind' amethibitisha mteja wake yuko huru baada ya mkataba wake kumalizika ambapo ifikapo Julai 15 watafanya tathmini ya ofa walizopokea mezani.
"Mwamnyeto amemaliza mkataba kwa sasa anamaliza majukumu yake ya kijamii ifikapo Julai 15 tutakaa mezani kuangalia ofa zilizopo"
"Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwake kwani aliweza kutwaa ubingwa na Yanga huku akifunga mabao katika mechi muhimu hivyo ni wazi kipaumbele cha kwanza ni kuongeza mkataba Yanga."
"Amekuwa Yanga kwa misimu sita sasa hivyo atakuwa tayari kuendelea kusalia kwa kuzingatia makubaliano na maslahi. Lakini kama hilo litashindikana tutaangalia ofa zilizopo na kufanya uamuzi," alisema Mastamind ambaye pia anamsimamia mchezaji mwingine wa Yanga Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr'.