Je ni mwisho wa enzi ya Farid Mussa na Yanga?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jul 2026
Je ni mwisho wa enzi ya Farid Mussa na Yanga?

Mkataba wa kiungo mshambuliaji na beki wa kushoto Farid Mussa Malik na klabu ya Yanga SC umefikia tamati, jambo linaloweka wazi uwezekano mkubwa wa nyota huyo kutokuwepo kwenye kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara kwa msimu ujao.

Baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa takribani miaka sita yenye mafanikio makubwa, Farid anabaki kuwa miongoni mwa wachezaji waandamizi waliogusa mioyo ya Wananchi kwa weledi, nidhamu na uvumilivu mkubwa.

Mwanzo wa Safari: Kuwasili Jangwani Mwaka 2020

Safari ya Farid Mussa ndani ya Yanga ilianza rasmi tarehe 12 Agosti 2020, pale uongozi wa klabu ulipotangaza kumsajili kama mchezaji huru baada ya kukamilisha kandarasi yake na CD Tenerife ya Hispania.

Wakati anajiunga na Yanga, klabu hiyo ilikuwa kwenye kipindi cha mpito cha kujenga kikosi kipya cha ushindani. Licha ya kuhusishwa kwa karibu na Simba SC, Farid alichagua kuvaa uzi wa njano na kijani, huku akicheza mechi yake ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi.

Tangu mwaka 2020 hadi sasa, Farid amekuwa mmoja wa wachezaji waliotumika kimkakati zaidi, ingawa msimu uliopita alipata nafasi finyu kwenye kikosi cha kwanza. Katika kipindi hicho, amefanya kazi chini ya makocha mbalimbali wenye falsafa tofauti, akiwemo Nasreddine Nabi ambaye alimpa nafasi kubwa zaidi kuliko makocha wengine waliofuata.

Mafanikio aliyopata Yanga

Katika kipindi chake cha utumishi, Farid amekuwa sehemu ya kizazi cha dhahabu kilichorejesha utawala wa Yanga kwenye soka la Tanzania na Afrika Mashariki. Amechangia mafanikio yafuatayo:

  • Mataji mfululizo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
  • Makombe ya CRDB Federation Cup.
  • Ngao za Jamii.
  • Kufika Fainali ya CAF Confederation Cup mwaka 2023.
  • Kufika Robo Fainali ya CAF Champions League.

Hatma yake ni ipi?

Kwa sasa Farid Mussa ni mchezaji huru (Free Agent) baada ya mkataba wake kumalizika rasmi. Ripoti zinaeleza kuwa hakuna mazungumzo yaliyoendelea kati yake na uongozi wa Yanga kuhusu kuongeza mkataba, jambo linalompa nafasi ya kusikiliza ofa kutoka klabu nyingine.

Baada ya miaka sita ya mafanikio akiwa Jangwani, huu unaweza mwisho wa zama baina yake nna Yanga lakini utumishi wake katika klabu hiyo kongwe zaidi nchini utaendelea kukumbukwa na Wananchi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’