Kocha Patrick Mabedi anatarajiwa kuondoka kunako klabu ya Yanga baada ya mkataba wake kumalizika.
Mabedi alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu uliopita kumuongezea nguvu Romain Folz aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema mabingwa hao wa soka Tanzania Bara hawataendelea nae kufuatia ujio wa kocha Manqoba Mngqithi ambaye atatua na benchi lake la ufundi.
Hata hivyo Kamwe amethibitisha kuwa kocha Abdihamid Moalin atajumuishwa kwenye benchi jipya Mngqithi akiwa mmoja wa makocha wadaidizi wawili.
Yanga pia iko kwenye mazungumzo na kocha wa viungoTshephang "Chyna" Mokaila ili kumuongezea mkataba likiwa ni pendekezo la Mngqithi.
Katika msimu wake mmoja na Yanga, Mabedi alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa kombe la Mapinduzi na kutetea ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa msimu wa tano mfululizo.