Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema katika usajili wa dirisha hili, Mfadhili/Mdhamini wa klabu hiyo Ghalib Said Mohamed 'GSM' ameweka fedha nyingi mezani ili kusajili wachezaji wenye ubora.
Kamwe amedokeza kuwa asilimia kubwa ya wachezaji waliosajiliwa katika dirisha hili Yanga imeingia gharama ya kuvunja mikataba yao.
"Bosi wetu GSM kama kuna msimu ametumia fedha nyingi ya usajili ni dirisha hili kwani sajili nyingi ambazo zimefanyika tumevunja mikataba"
"Nyingi tumenunua kwa maana ya kuvunja mikataba yao na kuwalipa wachezaji fedha. Tuna kila sababu ya kumshukuru GSM na Yanga tunajivunia uwepo wake."
"Umefanyika usajili mkubwa, tumewaongeza wachezaji wengi kwenye timu," alisema Kamwe.
Akizungumzia utambulisho wa nyota hao wapya, Kamwe amesema hakutakuwa na 'mbwembwe', wachezaji watatambulishwa kwa utaratibu uleule kama alivyotambulishwa kocha mkuu Manqoba Mngqithi.
"Safari hii hatutakuwa na mambo ya saa 8 usiku, tunafanya utambulisho wakati wowote, hatutatengeneza 'trending' kabla ya utambulisho hizo trending zenyewe zitafuata utambulisho wetu," aliongeza Kamwe