Abuya bado yupo sana Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jul 2026
Abuya bado yupo sana Jangwani

Klabu ya Yanga inaendelea na mchakato wa kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao huku pia wakihakikisha nyota muhimu wa kikosi cha kwanza wanaendelea kusalia.

Habari njema kwa Wananchi ni kuwa kiungo kiraka Duke Abuya ataendelea kusalia Jangwani kwa muda mrefu baada ya kuongeza mkataba.

Inaelezwa mkataba wa Abuya na Yanga ulikuwa umesalia mwaka mmoja lakini kutokana na thamani yake ya sasa, mabosi wa Yanga wamerudi mezani na kumuongeza mwaka mwingine mmoja ambapo sasa atasalia Jangwani hadi 2028.

Katika msimu uliopita, kama Yanga itatoa tuzo ya mchezaji bora wa msimu pengine tuzo hiyo itakwenda kwa Abuya.

Tangu alipojiunga na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea Singida BS, kiwango cha Abuya kimekuwa kikipanda msimu hadi msimu.

Uwezo wake wa kucheza nafasi zadi ya moja uwanjani uliinufaisha Yanga msimu uliopita. Muda mwingi alitumika kama kiungo mkabaji na aliitendea haki nafasi hiyo aliyoanza kuitumikia baada ya kuondoka Khalid Aucho.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’