Dondoo za kombe la dunia : Urusi v Saudi Arabia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jun 2018
Dondoo za kombe la dunia : Urusi v Saudi Arabia
Urusi wenyeji wa michuano ya kombe la dunia saa 12 jioni ya leo Alhamisi, Juni 14 2018 watashuka kwenye dimba la Luzhniki kuikaribisha Saudi Arabia kwenye mchezo ambao unaonekana kuwa 'rahisi' kwa wenyeji.

Hata hivyo wenyeji hao hawako vizuri kabisa kutokana na rekodi yao mbovu katika kipindi cha miezi nane iliyopita.

Urusi imecheza kwa miezi nane bila kushinda ambapo mchezo wa mwisho kuelekea michuano hiyo ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Uturuki ambayo haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia tangu mwaka 2002.

Lakini wanahitaji kushinda mchezo huo ili kuwapa imani mashabiki wao hasa ikizingatiwa wanacheza na Saudi Arabia ambayo haina historia nzuri kwenye michuano hiyo.

Urusi na Saudi Arabia hazijawahi kukutana kwenye mchezo wa kimashindano.

Mara ya mwisho zilikutana mwaka 1993 kwenye mchezo wa kirafiki ambapo Saudi Arabia ilishinda kwa mabao 4-2.

Tangu kuvunjika kwa USSR, Urusi imefuzu mara tatu kwa michuano ya kombe la dunia (1994, 2002, 2014) na haijawahi kufuzu kwenda raundi ya mtoano.

Urusi imecheza michezo mitano mfululizo ya kombe la dunia bila ya kushinda(D2,L3).

Ushindi pekee wa michezo miwili iliyopata kwenye michuano hiyo ni dhidi ya timu kutoka Afrika (6-1 dhidi ya Cameroon mwaka 1994 na 2-0 dhidi ya Tunisia mwaka 2002)

Katika michuano hii kocha wa Urusi Stanislav Cherchesov huenda akatumia mfumo wa 4-1-4-1. Kocha huyo amemuongeza kikosini mlinzi Sergei Ignashevich mwenye umri wa miaka 38 na anatarajiwa kuongoza safu ya ulinzi.

Kiungo Aleksandr Golovin ndiye anayeterajiwa kuibeba Urusi huku Alan Dzagoev akitarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji.

Kwa upande wa Saudi Arabia, inashiriki michuano ya kombe la dunia kwa mara ya tano, mwaka huu wakiwa wamerejea baada ya kushindwa kufuzu mwaka 2010 na 2014.

Saudi Arabia imemaliza mkiani katika makundi awamu tatu zilizopita. iliwahi kufuzu hatua ya mtoano mwaka 1994 pekee ambapo walifungwa na Sweden hatua ya 16 bora.

Saudi Arabia imekwenda Urusi kushiriki michuano hii bila mshambuliaji wake tegemeo Nawaf Al-Abed aliyeondolewa kikosini dakika za majeruhi baada ya kuumia.

Mfumo wanaotumia Saudi Arabia ni 4-3-2-1 ikitegemea mashambulizi ya kushitukiza kupitia kwa washambuliaji wake wenye kasi Salem Al-Dawsari na Fahad Al-Mullawad
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’