Kiungo kinda aliyesajiliwa na Yanga kutoka klabu ya JKU ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk 'Mpemba D', jana alikuwa sehemu ya wachezaji walioanza kujifua kwenye maandalizi ya pre-season chini ya kocha mkuu Manqoba Mangqithi.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18 ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na mabingwa hao wa nchi kwenye dirisha hili.
Bado nyota huyo hajatambulishwa rasmi lakini taratibu zote za usajili wake zimekamilika.


ADVERTISE HERE