Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema bado kuna wachezaji wawili wa kigeni wanasubiri utambulisho ili kukamilisha usajili wa Kimataifa msimu huu.
Mpaka sasa Yanga ina wachezaji 11 wa kigeni wanaoendelea kujifua Avic Town katika maandalizi ya msimu mpya 'pre-season'.
Usajili huo wa wachezaji wawili zaidi utaifanya Yanga iwe na wachezaji 13 ambapo italazimika kumtoa mchezaji mmoja ili kusalia na wachezaji 12.
Nyota saba wa kigeni waliobaki kwenye kikosi cha msimu uliopita ni Djigui Diarra, Yao Kouassi, Chadrack Boka, Duke Abuya, Maxi Nzengeli, Allan Okello na Laurindo Aurelio 'Depu'.
Nyota hao wanaungana na wanne waliotambulishwa mpaka sasa wakisajiliwa kwenye dirisha hili ambao ni Cheick Ibrahim Toure, Housseine Zakouani, Albert Kangwanda na Peter Shalulile.
Ni wazi kama wataongezwa wengine wawili, Yanga italazimika kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni, je ni nani? Ukiangalia safu ya ushambuliaji ndio inaonekana kuwa na utajiri mkubwa wa wachezaji na pengine huenda panga likapita katika eneo hilo.