Leo Jumamosi, August 1 2026 Rais wa Yanga Injinia Hersi Said atakata mzizi wa fitna kwa kumtambulisha mchezaji namba 6 ambaye kwa wiki kadhaa sasa Yanga imefanya maandalizi ya ujio wake.
Saa 5 usiku Injinia Hersi atazungumza na wanahabari kumuweka hadharani mchezaji huyo. Lakini sio mmoja! kuna wachezaji wawili wa kigeni wanakwenda kutambulishwa huku taarifa za ndaani zikidokeza kuwa kunaweza kuwa na 'sapraizi' ya mchezaji mwingine wa ndani.
Aidha, upitia mazungumzo hayo, huenda Injinia Hersi akaweka hadharani hatma ya mchezaji mmoja wa kigeni ambaye atahitaji kupunguzwa ili kusalia na wachezaji 12 baada ya usajili wa nyota hao wawili wapya wa kigeni.
Ni saa 5 usiku leo...!
ADVERTISE HERE