Kikosi cha Yanga kesho Jumanne saa 4 asubuhi kitaelekea Geita kwa ajili ya kwenda kushiriki uzinduzi wa uwanja wa Biteko Stadium uliopo Ushirombo.
Kikosi kitashukia Kahama kisha itaanza safari nyingine kuelekea Ushirombo.Β
Wachezaji wa Yanga wanatarajiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja huo baada ya tukio la uzinduzi wa wiiki ya Mwananchi kukamilika.
Yanga haitacheza mechi ya kirafiki ambapo kikosi kitarejea jijini Dar es salaam siku hiyohiyo baada ya zoezi hilo kukamilika.
Wananchi wataendelea na maandalizi yao Avic Town kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi August 09 katika uwanja wa Uhuru.
ADVERTISE HERE
