Mshambuliaji mpya wa Yanga Peter Shalulile 'Shasha 'Man' amewashukuru mamia ya mashabiki wa Yanga waliojitokeza Makao Makuu ya klabu hiyo Jangwani kumkaribisha.
Hafla ya mapokezi ya mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Namibia iliongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said.
"Nawashukuru nyote mliofika hapa kunipokea, nimependa ari na morali mliyonayo. Ninawaahidi nitapambana ili kuhakikisha tunashinda mataji. Najua sitakuwa peke yangu, ni ushirikiano kati yetu wachezaji na nyinyi mashabiki," alisema Shalulile ambaye utambulisho wake ulirushwa mbashara na Azam TV
Ujio wa mfungaji huyo bora wa muda wote ligi kuu ya Afrika Kusini, umemaliza uvumi uliokuwa unasambazwa na baadhi ya watu kuwa Yanga haikumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns na kuwa alikuwa akitumika kwa ajili ya masuala ya uchaguzi.