Yanga na mpango wa utambulisho wa staa mkubwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Aug 2026
Yanga na mpango wa utambulisho wa staa mkubwa

Kuna imani kuwa nyota ambaye anazungumziwa na viongozi wa Yanga kuwa anaweza kusajiliwa kabla ya drisha la usajili kufungwa ni Feisal Salum 'Fei Toto'

Hata hivyo, Bilionea GSM atalazimika 'kuvunja benki' ili kukamilisha usajili wa kiungo huyo ambaye historia yake ya mafanikio kwenye soka hapa nchini ilianza wakati yuko Yanga.

Fei Toto bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Azam Fc ambapo matajiri hao kutoka Chamazi wanamuona bado ni mchezaji muhimu kwenye mipango yao wakihitaji zaidi ya Bil 6 kumuachia.

Baada ya mpango wa kumrejesha Stephane Aziz Ki kukwama, Yanga inaonekana kuweka nguvu kwa Fei Toto wakilenga kuimarisha eneo la viungo washambuliaji. Kwa sasa Yanga inamtegemea Allain Okello zaidi katika nafasi hiyo.

Jana Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alidokeza usajili wa mchezaji ambaye alidai kwa sasa anafanya mazoezi na timu yake lakini sio mchezaji wao. Kamwe alisema mpango wa kumtambulisha mchezaji huyo unakwenda sambamba na uzinduzi wa jezi.

Msemaji huyo wa mabingwa wa nchi alisema hadi kufikia siku ya Ijumaa jezi mpya kwa ajili ya 2026/27 zitazinduliwa na pengine katika tukio la uzinduzi, nyota huyo atatangazwa.

Kuchelewa huko kunatafsiriwa kama mpango wa Yanga kumtumia mchezaji huyo kwenye utambulisho wa jezi na ikiwezekana kuandaa jezi maalum zenye jina lake ambazo zitauzwa baada ya kutambulishwa kama zifanyavyo timu kubwa barani Ulaya.

Juventus wakati wa utambulisho wa Cristiano Ronaldo alipojiunga na timu hiyo, waliuza maelfu ya nakala za jezi maalum zenye jina la CR7 ikielezwa walirudisha fedha walizotumia kumn'goa Real Madrid ndani ya siku moja tu kwa kuuza jezi.

Tukio kama hilo pia lilifanywa na PSG pale walipomsajili Lionel Messi kutoka klabu ya Fc Barcelona wakiuza maelfu ya jezi maalum iliyokuwa na jina lake.

Je Yanga inalenga kutumia utaratibu huo kwenye utambulisho wa mchezaji huyo ambaye wanadai usajili wake utatikisa nchi?

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’