Droo ya hatua ya awali na raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho (CAFCC) imefanyika leo huko Cairo, Misri.
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamepangwa kuanza dhidi ya Gaborone United mchezo wa hatua ya awali.
Wananchi wataanzia ugenini mechi ya kwanza na kumalizia mechi ya pili nyumbani.
Endapo Yanga itashinda mchezo huo wa hatua ya awali, raundi ya kwanza watakutana na mshindi wa mchezo kati ya CFFA Fc ya Madagascar dhidi ya Lijabatho Fc ya Lesotho.
Mechi za hatua ya awali zitapigwa kati ya Septemba 4-6, 2026 na marudiano kati ya Septemba 11 - 13 mwaka huu.
ADVERTISE HERE
