Kamwe afunguka Yanga imefungiwa kusajili?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Aug 2026
Kamwe afunguka Yanga imefungiwa kusajili?

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametoa ufafanuzi wa taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Yanga kufungiwa kusajili kwa madirisha matatu.

Kamwe amesema jambo hilo lilikuwa changamoto ya kawaida kwenye mfumo wa usajili wa FIFA na kuwa tayari limepatiwa ufumbuzi.

"Michakato yote ya usajili inafanyika kwenye mfumo wa FIFA ambao unahusisha zaidi ya pande moja katika kukamilisha mchakato mzima"

"Tukimsajili mchezaji kuja timu yetu, tutaingiza taarifa na nyaraka zote kwenye mfumo ikiwemo mkataba na taarifa ya malipo ambayo tumefanya kwa mchezaji pamoja na klabu yake. Na wao waliotuuzia mchezaji wanatakiwa wathibitishe kwenye mfumo kuhusu taarifa za mkataba na malipo yaliyofanyika."

"Ikitokea pande moja ikakwamisha mchakato, mfumo wa FIFA utabaini kuwepo changamoto. Kuna moja ya klabu haikuwa imethibitisha viambatanisho vya malipo ambavyo tulikuwa tumeviweka na hivyo kupelekea sintofahamu iliyojitokeza"

"Pengine ni kwa sababu Yanga ni klabu kubwa jambo hili limechukuliwa kama ni kubwa sana, kila siku Yanga anafungiwa kusajili, kila siku Yanga anasajili na kila siku Yanga anakuwa bingwa"

"Kwa mujibu wa CEO, timu husika ilitafutwa ikathibitisha kufanyika kwa malipo hayo na hivyo changamoto hiyo tayari imepatiwa ufumbuzi," alisema Kamwe

Katika hatua nyingine, Kamwe amethibitisha kuwa klabu ya FC Les Aigles du Congo itachuana na Yanga siku ya Jumapili kwenye mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 1:30 usiku.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’