Mabula yuko Dar, anatua Yanga?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Aug 2026
Mabula yuko Dar, anatua Yanga?

Kiungo mkabaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Alphonce Mabula amerejea nchini akitajwa kuwa mbioni kujiunga na mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga.

Mabula amehusishwa sana na Yanga kwenye dirisha hili la usajili taarifa zikibainisha kuwa makubaliano ya kutua kwa Wananchi yalishafikiwa suala lililokuwa limebaki ni kusaini mkataba tu

Kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania ana uzoefu mkubwa wa soka la nje baada ya kutumia takribani misimu minne akicheza Ulaya. Kabla ya kujiunga na Shamakhi ya Azerbaijan Januari 2025, Mabula alikuwa sehemu ya kikosi cha Spartak Subotica ya Serbia aliyojiunga nayo Februari 2022 akitokea Alliance FC.

Mbali na Spartak Subotica, Mabula pia aliwahi kucheza RFK Novi Sad kwa mkopo katika msimu wa 2024/25, akipata uzoefu zaidi katika mazingira ya soka la ushindani barani Ulaya.

Uwezo wa Mabula kucheza nafasi mbalimbali za kiungo ni moja ya vitu vilivyoivutia Yanga. Mbali na kuwa na uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji, nyota huyo pia anaweza kusaidia katika ujenzi wa mashambulizi kutokana na uelewa wake wa mchezo.

Ingawa ni mchezaji wa ndani, uzoefu wake wa kucheza mashindano ya kimataifa na soka la ushindani nje ya Tanzania umetajwa kuwa sababu kubwa iliyowafanya viongozi wa Yanga kuvutiwa na huduma yake.

Kuna sapraizi imeandaliwa kwa Wananchi siku ya Jumapili kwenye YANGA DAY, huenda jina la Mabula likatangazwa kutua kwa Wananchi siku hiyo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’