Kiungo Mohamed Damaro 'Ngosha' ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kutambulishwa leo kuwa sehemu ya jeshi la Yanga kuelekea msimu wa mashindano 2026/27.
Kulikuwa na tetesi nyingi kuhusu hatma yake, urejeo wake ni ishara kuwa mabosi wa Yanga wamempa mkataba mpya baada ya mkataba wake wa mkopo kutoka Singida BS kumalizika.
Damaro alichelewa kujiunga na kikosi cha Wananchi akipewa mapumziko zaidi baada ya kufunga ndoa wiki iliyopita huko Guinea.
Ndio! Ngosha bado yupo mikononi mwa Wananchi...!
ADVERTISE HERE