Hersi amemsajili Mwalimu 'kibabe'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Aug 2026
Hersi amemsajili Mwalimu 'kibabe'

Inaelezwa mshambuliaji mpya wa Yanga Suleiman Mwalimu alirejea nchini jana akitokea klabu ya Wydad CA ya Morocco kwa lengo la kujiunga na Simba.

Simba iilikamilisha taratibu zote za kumsajili Mwalimu kwa mkopo ambapo ni wao waliofanya taratibu za kumsafirisha kutoka Morocco na wakampokea jijini Dar es salaam.

Baada ya kutua Dar Mwalimu akasafiri visiwani Zanzibar ambapo jioni akajiunga na kikosi cha Simba na akafanya mazoezi na jioni na timu hiyo.

Hakuishia hapo, Mwalimu akashiriki program nyingine za timu muda wa usiku ikiwa ni pamoja na kupata chakula cha pamoja na wachezaji wenzake.

Hata hivyo Yanga tayari ilikuwa na taarifa kuwa licha ya Simba kufikia makubaliano na Wydad, walikuwa hawajalipa fedha ili kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania.

Mahusiano mazuri kati ya Rais wa Yanga Injinia Hersi Said na viongozi wa Wydad, yakatoa mwanya kwa Injinia kupata taarifa sahihi na hivyo kukamilisha mchakato wa kumsajili mshambuliaji huyo kwa mkopo wa msimu mzima na muda huo wa usiku Mwalimu akasafiri kutoka Zanzibar hadi Dar es salaam kusaini mkataba.

Viongozi wa Simba wameshikwa na butwaa wasielewe nini kimetokea kwani mchezaji waliikuwa nae mpaka usiku lakini asubuhi wakakutana na picha za utambulisho kwenye kurasa za Yanga..!

Usajili wa Mwalimu ni sehemu ya 'vita' kubwa ya kuchukuliana wachezaji kati ya Yanga na Simba ambayo haijaanza leo.

Wengi hawajasahau kilichotokea kwa Bernard Morrison misimu michache iliiyopita licha ya kuwa baadae Yanga ilimsajili tena Morisson.

Hata Rais mstaafu awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete aliwahi kusema vita hii ni miaka na miaka na unapochukuliwa mchezaji usilalamike na wewe jipange ukachukue wa kwao.

Tangu tukio la Morisson, Yanga imejipanga vyema ambapo baada ya kuwasajili Jonas Mkude, kumrejesha Morrison, kumsajili Clatous Chama na Mohamed Hussein ''Zimbwe Jr' msimu uliopita, msimu huu wamepita na Mwalimu katika usajili ambao pengine unaweza kuwauma zaidi Simba kwani ni mchezaji alikuwa mchezaji muhimu kwenye mipango yao.

Ni juzi tu walimtambulisha kwenye Tamasha lao la Simba Day lakini leo ni Mwananchi...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’